MWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA

MWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA

UTANGULIZI


MWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA

“Kidagaa Kimemwozea” ni kitabu chenye jalada jeusi iliyorembeshwa kwa picha ya mwanamwali mmoja mrembo aliyekuwa akidondoshwa na machozi. Riwaya hii ni aina ya kipekee,inayothibitisha usanii wa kupigiwa mfano jinsi ndoto ya uhuru barani Afrika ilivyogeuka kuwa jinamizi inayowafanya wazalendo kulia, “kidagaa kimetuozea” kwa kutamaushwa na usaliti wa viongozi wa baada ya Uhuru.


Hapa twafahamu kuwa kidagaa kilichokuwa kimeoza kiliwaozea wanyonge haswa, kwa kupitia wahusika kama Amani, Imani, Uhuru, DJ, Matuko n.k. wahusika hawa pamoja na wengine ndio wale wanaodhulumiwa na viongozi wao ambao, badala ya kuonyesha uongozi mwema, wanaongoza kwa kuwatesa na kuwanyang’anya na hata kuwaua wananchi wanaofaa kuwalinda.


Hadithi hii imetolewa kupitia safari ya wahusika wawili, Amani na Imani. Wawili hawa wanang’oa nanga kutoka mastakimunini mwao kuelekea mji wa Sokomoko ili kutafuta kazi zitakazowafanya kuishi maisha ya faraja na yenye buheri wa afya.


Hata hivyo katika safari yao, wanafika ukingoni mwa mto Kiberenge ambao maji yake yanasitishwa na wenyeji kwa tuhuma kuwa ni maji ya kifo. Amani na Imani wanavunja mwiko huu kwa kuyanywa maji haya. Tendo hili ambalo Imani anadai kuwa ni kuhalilisha yaliyo haramu linawashangaza wenyeji ambao kwa kuogofya matokeo yake, wanagundua kuwa waili hawa hawaathiriki kivyovyote vile.


Click here to download wholeMWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA