MWONGOZO WA CHOZI LA HERI

MWONGOZO WA CHOZI LA HERI

MWONGOZO WA CHOZI LA HERI


Click here to download wholeMWONGOZO WA CHOZI LA HERI

JALADA


Jalada la Riwaya ya Chozi la Heri ni tokeo la usaniiwake , Robert Kambo. Katika upande wa mbelesehemu ya juu, mna rangi ya kijani kibichi iliyokolea.
Maana ya rangi hii ni uhai na rutuba. Riwayani yamo maeneo yaliyo na rutuba yanayotoa mazao mengi.

Katika eneo la Msitu wa Heri alikoishi Ridhaa kwamiongo mitano, mwanzoni kulikuwa kama jangwa laKalahari lakini Ridhaa alihakikisha kuwa kijiji hiki
kimepata maji ya mabomba hadi eneo zima likatwaarangi ya chanikiwiti. Miti mingi kama Miambakofi, mivule na miti mingine kapandwa. Maeneo mengme yaliyokuwa na rutuba ni kamaMsitu wa Mamba.

Watu waliogura makwaowalipohamia hapa walikata miti na kupanda vyakulakama mahindi ambayo yalifanya vizuri mno.Ndam ya rangi hii mna anwani ya kazi iliyoandikwakwa rangi nyeupe. Kawaida rangi hii huashiria amani. Licha ya mambo kuwaendea vibaya wahusika wengi riwayani, hatimaye mnaamani ya kudumu.

Jina lake mwandishi liko maeneo yayo hayo nalimeandikwa kwa rangi ya manjano. Rangi hii huashira ukomavu. Mwandishi wa riwaya hii ni mwenye tajriba pana. Amekomaa katika uandishi wa kazi za fasihi. Masuala anayoyaangazia ni yale
yanayoiathiri jamii yake. Ametumia mtindo unaoashiria upeo wa ukomavu wake.

Upande wa chini wa jalada la riwaya hii mna mchoro wa jicho. Jicho hili linadondokwa na chozi. Ndani ya chozi mna watu watatu(mmoja wa kike na wawili wa
kiume). Inahalisi kuwa watu hawa watatu ni Umu, Dick na Mwaliko. Walifurahl mno walipokutana wotekatika hoteli ya Majaliwa. Riwayani, Umu na Dickwalikimbia wote kwa pamoja na wakamkumbatiandugu yao Mwaliko na huku wakaanza kulia nakutokwa na machozi ya faraja heri.

Click here to download wholeMWONGOZO WA CHOZI LA HERI