Isimu jamii – Ni taaluma inayochunguza uhusianouliopo baina ya lugha na jamii. Hasa hushughulikia jinsi watu wanavyotumia lugha katika jamii. Isimu- ni uchunguzi wa lugha kisayansi.
Jamii – ni kundi filani la watu wenye uhusiano fulani.
Mambo yanayoshughulikiwa katika isimu jamii
i) Tofauti katika lahaja za lugha kama vile Kiswahili cha lamu(kiamu), cha Mombasa(kimvita), cha unguja(kiunguja), cha bara. ii) Tofauti katika matumizi ya lugha baina ya makundi tofauti tofauti katika jamii. Mfano wazee na watoto,vijana na wabunge. iii) Matumizi ya lugha kutegemea miktadha tofauti kama vile kazini, nyumbani, sokoni, n.k. iv) Mtazamo wa watu kuhusu lugha. Je, wanaitukuza au wanaitweza? v) Jinsi mtu anavyotumia lugha kutegemea uhusiano na wazungumzaji au mada husika.
Lahaja mbalimbali za lugha ya Kiswahili.
i) Huwafunza watu kaida za lugha ili waweze kuitumia ipasavyo kutegemea mila na desturi. ii) Humsaidia mzungumzaji au mwandishi kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na usahihi. iii) Humpa anayetumia lugha uwezo wa kutambua, kutofautisha na kutumia mitindo mbalimbali ya lugha kutegemea mahitaji. iv) Hufunza maadili ya jamii hasa yanayohusiana na matumizi ya lugha kutegemea uhusiano. Mf. Mtu na mkwewe, mtoto na mzazi, mwajiri na mwajiriwa. v) Hufunza mbinu za mawasiliano pamoja na mbinu za kupata maana kamili. vi) Hudhihirisha utamaduni wa jamii. vii) Humsaidia msemaji au mwandishi kutambua makosa mbalimbali yanayojitokeza wakati wa kuzungumza au kuandika. viii) Hufunza mbinu za kuwaelewa watu tunaotagusana nao kwa kuzingatia mambo k.v hadhi, utamaduni hivyo utangamano.
Maana ya mawasiliano.
Utaratibu ambao huwawezesha viumbe kupashana ujumbe ambao unahusisha mwasilishi na mpokeaji wa ujumbe.
Njia ambazo kwazo mwanadamu huwasiliana.
i) Mgusano na ukaribianaji ii) Mavazi iii) Sauti iv) Ishara za mwili.
Ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na wanadamu katika mawasiliano.
Sifa za lugha.
i) Hakuna lugha iliyo bora kushinda zingine. –zote ni sawa. ii) Kila lugha ina sifa zake. iii) Lugha hubadilika kutegemea mazingira, aina ya tukio, wakati na matumizi ya lugha hiyo. iv) Lugha ina uwezo kukua, mfano Kiswahili kimebuni msamiati TEHAMA (Teknolojia ya habari na mawasiliano.)
v) Lugha pia hufa kwa msamiati wake kupotea n.k
(i) Lugha moja kusonewa hadhi na isiyoonewa hadhi hufifia. (ii) Sababu za kiuchumi – watu huishi mijini na kuacha lugha ya kwanza. (iii) Lugha kuwa na idadi ndogo ya wazungumzaji. (iv) Ndoa za mseto. (v) Kuhamia kwingine – watu huishi na kuingiliana na kundi jingine. (vi) Mielekeo ya watu – wanapoipendelea lugha moja na kuidharau nyingine.
(vii)Kisiasa – Lugha moja kupendelewa kuliko nyingine na viongozi. Umuhimu wa lugha.
i) Hutumika kwa mawasiliano. ii) Lugha ni chombo ambacho hutusaidia kujieleza na kutoa mawazo yetu. iii) Hujenga uhusiano baina ya watu. iv) Ni kitambulisho cha taifa, mtu binafsi na utamaduni. v) Lugha ni chemchemi ya uchumi mf. Mtangazaji au mwalimu wa Kiswahili. vi) Huweza kuunganisha watu kama jamii moja.